SHARE

Majaribio ya kulipua silaha za nyuklia angani – ikiwa ni pamoja na 500 yaliyofanyika kuanzia 1945 hadi 1980 – yalikuwa hasa na athari mbaya, yakasambaza chembe nururishi mbali na katika sehemu pana. Silaha zote hizo zikichanganywa zilikuwa na uwezo wa kuharibu ulio sawa na wa mabomu 29,000 ya nyuklia kama lililongushwa Hiroshima.

Hivi leo, kila mtu aliye hai anabeba ndani ya mwili wake chembe nururishi kutoka kwa majaribio yanayofanywa angani na hivyo kuongeza hatari ya magonjwa. Madaktari wa matibabu wanabashiri kwamba baada ya muda, majaribio yaliyopita yatasababisha vifo vya mapema visivyopungua milioni nne kutokana na kansa na magonjwa mengine.

Majaribio ya kulipua silaha za nyuklia baharini na chini ya ardhi yamekuwa pia na madhara ya muda mrefu kwa afya na mazingira.

Kwa kujali kuhusu athari za majaribio ya silaha za nyuklia ulimwenguni, maandamano makubwa katika sehemu nyingi za dunia yalifanyika mwisho mwisho wa nusu ya kwanza ya karne ya 20. Maandamano hayo yalilazimisha viongozi kushauriana kuhusu upigaji marufuku kwa kiasi wa silaha hizo mnamo 1963. Uharamishaji kamili mnamo 1996 ulifuatia. Hatua hizo mbili zimesaidia kuzuia majaribio ya silaha za nyuklia ulimwenguni.

Lakini athari za majaribio ya mapema kwa maisha ya watu na mazingira dhaifu zitaendelea kuonekana kwa vizazi vijavyo. Jamii ya kimataifa ina jukumu sio tu la kuhakikisha kwamba uharibifu kama huo hautokei tena lakini kujitahidi pia kuakisi madhara yaliyotendeka.

Manusura wachache wa majaribio ya silaha za nyuklia popote ulimwenguni wamefidiwa kwa mateso yao, na juhudi za kusafisha maeneo ya zamani ya kufanyia majaribio hazitoshi. Katika baadhi ya maeneo, maporomoko ya majengo na miundo msingi mingine ni hatari inayoendelea ya utoaji sumu zaidi.

Mlipuko wa majaribio uliofanywa 1971 na Ufaransa katika Moruroa Atoll iliyomo Mā’ohi Nui. Picha na: Serikali ya Ufaransa

Shimo la katikati ya mlima lililochimbuliwa na mlipuko wa jaribio la bomu la nyuklia lililofanywa na Russia katika Kazakhstan. Picha na: CTBTO