SHARE

Urithi wa majaribio ya nyuklia

Ili kuimarisha uharibifu na uwezo wa kuua wa nguvu za nyuklia walizonazo, na kutoa onyo kwa washindani wao, mataifa yenye silaha za nyuklia yamefanya majaribio zaidi ya 2,000 ya kulipua silaha za nyuklia kote ulimwenguni tangu 1945.


Kwa kuachilia hewani na baharini kiasi kikubwa cha mnururisho, majaribio hayo ya sumu yamesababisha majanga ya kansa na magonjwa mengine ya kudumu. Maeneo makubwa ya ardhi yangali si salama kuishi, hata baada ya miongo mingi ya kufungwa kwa maeneo ya majaribio.

Wiki tatu baada ya mashambulizi ya mabomu ya nyuklia katika Hiroshima na Nagasaki, Serikali ya Marekani ilifanya jaribio la kwanza la kulipua silaha za nyuklia katika Jimbo la New York, zoezi lililopewa jina la siri “Trinity”. Moto mkubwa kutoka kitovu cha mlipuko wa bomu uligeuza mchanga kuwa vioo, ukaangaza milima ya karibu na kurusha wingu la mabaki ya nururishi lenye umbo la uyoga umbali wa kilomita 12 hewani.

Waliokuwa wakifanya kazi katika maeneo ya majaribio na jamii jirani walipatwa na uharibifu mkuwa ambao athari zake zinaendelea kuonekana mpaka wa leo.

Hali imekuwa ni hiyo hiyo kwa wanaofanya kazi ama kuishi katika sehemu unakoelekea upepo na mito katika maeneo mengine zaidi ya 60 ulimwenguni ya kufanyia majaribio ya silaha za nyuklia, kuanzia jangwani za Australia na Algeria hadi maeneo makubwa yenye nyasi ya Kazakhstan na visiwa vya matumbawe vya Pacific.

Iroji Kebenli, akiwa na umri wa miaka 13 alipopata majeraha ya kuchomwa na nururishi wakati Marekani ilipofanya jaribio la silaha ya nyuklia katika Visiwa vya Marshall mnamo 1954. Picha na: Serikali ya Marekani

Wingu lenye umbo la uyoga kufuatia mlipuko wa majaribio wa bomu la nyuklia. Picha na: Serikali ya Marekani