SHARE

Si adilifu, ni haramu na kinyume na misingi ya kidemokrasia

Silaha za nyuklia husababisha maafa mengi na uharibifu mkubwa, na ni tisho kubwa kwa Maisha ya binadamu. Mauaji ya kiholela na kulemazwa kwa mamia ya maelfu ya watu hazina msingi wowote wa uadilifu.

Utumiaji wowote wa silaha za nyuklia unafaa kuwa ni kinyume cha sheria za kimataifa na uchukuliwe kuwa kosa kubwa la uhalifu wa kivita. Silaha zozote ziletazo maangamizi haziwezi kuwa na matumizi halali ya kijeshi au vitani.

Kura ya maoni kote ulimwenguni, ikiwa ni pamoja na nchini zenye silaha za nyuklia, zinaonyesha kuungwa mkono na wengi kwa marufuku ya silaha hizo. Serikali zinazoendelea kuunda silaha za nyuklia zinafanya hivyo kinyume kabisa na mapenzi ya raia wake.

Kila mtu, popote alipo, atanufaika kutokana na kumalizwa kwa silaha hizo za kuogofya.