SHARE

Kitovu cha milipuko

Katika kila jiji, waliokuwa karibu na kitovu cha milipuko, walikuwa na nafasi ndogo sana ya kunusurika. Karibu kila mtu aliyekuwa umbali wa katika kilomita 1.2 kutoka kwenye kitovu na ambaye hakuwa amejikinga kwa vyovyote na athari za bomu alikufa papo hapo ama baada ya wiki kadhaa.

Halijoto ardhini kwenye kitovu ilifikia digrii kati ya 3,000 na 4,000 kwa vipimo vya Celsius, huku watu waliokuwa umbali wa kilomita hadi 3.5 wakipatwa na majeraha ya kuchomeka. Mitetemeko mizito iliharibu karibu majengo yote ya mbao ndani ya umbali wa kilomita mbili.

Hata katika umbali wa kilomita moja, watu waliopata kiasi kikubwa cha mnururisho unaobadilika kuwa chuma na kuingiza sumu mwilini walikufa. Watu wengi waliokuwa mbali zaidi waliaga dunia kutokana na athari za baadaye za kupatwa na mnururisho.