Athari za silaha za nyuklia
Joto
Silaha ya nyuklia ikilipuliwa, hutoa joto kali. Karibu kila kitu na kila mtu katika kitovu cha mlipuko hugeuka mara moja kuwa jivu na mvuke.
Wimbi kubwa la moto ambao kipimo cha halijoto ya kitovu chake huwa ni zaidi ya digrii milioni moja kwa vipimo vya Celsius, hupaa juu angani na halijoto chini ardhini hufika digrii maelfu kadhaa na huwa juu zaidi kuliko ya jua.
Joto hilo kali huwasha moto unaoenea mbali, unarusha moshi wenye sumu hewani pamoja na gesi zinazoweza kuunguza. Moshi na gesi hizo zikiungana husababisha dhoruba au mvua kubwa ya moto.
Hata watu walio umbali wa makumi ya kilomita kutoka eneo la mlipuko wa bomu la nyuklia hupata majeraha kali na hatari ya kuchomeka yawezayo kuua, ilhali walio mbali zaidi hupoteza uwezo wa kuona kutokana na nuru kali ya silaha hizo.
[END]
Mlipuko
Silaha ya nyuklia hutoa pia ukuta mkubwa unaoenda kasi wa mvuke wenye nguvu nyingi ujulikanao kama wimbi la kishindo linalosafiri mbali kwa kilomita nyingi.
Wimbi hilo hurusha watu hewani, linawakosesha fahamu, linapasuapasua miili yao na kuharibu mapafu kabisa.
Majengo katika maeneo makubwa hubomolewa na watu wengi hupondwa na kuachwa maiti. Vitu vingine vilivyofunguka hupeperushwa angani kama makombora.
Hata magorofa makubwa yaliyokorogewa na mengine ya chuma huharibiwa na nguvu za mlipuko.
[END]
Mnururisho
Mfululizo wa madhara yanayosababisha mlipuko hutoa kiasi kikubwa cha mnururisho unaobadilika kuwa ioni, unapenya ndani ya miili ya watu, unaharibu au unadhuru viini vyao na kusababisha magonjwa.
Hata katika umbali wa kilomita kadhaa kutoka eneo la mlipuko, watu hupata mnururisho mkubwa kiasi cha kusababisha vifo kutokana na sumu yake kali.
Ishara zake ni pamoja na kutapika, ufizi wa meno kuvuja damu, kuharisha na nywele zote kung’oka. Waathiriwa wengi hufa miezi michache baada ya shambulizi.
Baadhi ya wanaopatwa na madhara hayo hupona lakini hufa baada ya miaka kadhaa au hata miongo kutokana na kansa na magonjwa mengine yanayohusishwa na madhara ya muda mrefu ya mnururisho.
Baadhi ya manusura huonyesha kasoro za kromosomu, na madhara mengine ya kinasaba yawezayo kupasishwa vizazi vijavyo.
[END]
Cheche za mnururisho zinazotokana na mlipuko wa bomu la nyuklia
Silaha ya nyuklia husababisha pia wingu kubwa lenye umbo la uyoga ambalo hunyonya vumbi na takataka zenye uwezo wa kunururisha, zinakuwa kama mnara wa cheche, na kurushwa hewani.
Mkondo wa upepo hutawanya cheche hizo hewani na hatimaye zinaanguka duniani na kuenea pakubwa.
Cheche hizo za mnunurisho zinazotokana na mlipuko wa silaha ya nyuklia husababisha hatari za afya hapo hapo na pia baada ya muda mrefu hata kwa watu walio mbali na kitovu cha mlipuko. Baadhi ya atomi nururishi huendelea kuwa hatari kwa muda mrefu, zinachafua udongo, maji na bidhaa za chakula.
[END]
Sumaku umeme
Silaha ya nyuklia ikilipuliwa katika maeneo ya juu, hutoa mapigo mazito ya sumaku umeme ambayo huharibu vifaa vya kielektroniki katika sehemu kubwa. Mawasiliano ya simu, uwezo wa kutumia intanet na teknolojia za huduma za benki huvurugwa kabisa.
Madhara hayo yalionekana kwa mara ya kwanza katika enzi ya majaribio ya silaha za nyuklia angani na maeneo yaliyo juu kutoka usawa wa bahari. Marekani ilipofanya jaribio la kulipua silaha ya nyuklia katika anga za juu umbali wa kilomita 400 juu ya kisiwa cha matumbawe cha Johnston katika Bahari ya Pacific, mlipuko uliharibu taa za barabara na simu katika Hawaii, umbali wa zaidi ya kilomita 1,450.
[SPLIT]
[VIDEO]https://assets.nationbuilder.com/ican/pages/13212/attachments/original/1778862539/video-explosion.mp4?1778862539[/VIDEO]
[CAPTION]Athari za mlipuko katika jaribio la kulipua silaha za nyuklia kwenye jumba la majaribio lililopo Jimbo la Nevada, Marekani. Picha na: Serikali ya Marekani[/CAPTION]