SHARE

Mataifa yanayokula njama za kudumisha silaha za nyuklia

Ingawa ni mataifa tisa yenye silaha za nyuklia, mengine zaidi ya 30 yanaunga mkono kubakizwa kwa silaha hizo na uwezekano wa kuzitumia, ikiwa ni pamoja na madai ya kulindwa na ‘mwavuli wa kinyuklia’ wa nchi marafiki zenye hifadhi za nyuklia.

Kwa mfano, mataifa yote wanachama wa Umoja wa Kujihami wa Nchi za Ulaya (NATO), yameidhinisha hadharani silaha za nyuklia. Baadhi yao yameipatia Marekani hifadhi ya mabomu ya nyuklia katika nchi zao – ikiwa ni pamoja na Ubelgiji, Ujerumani, Italia, Uholanzi na Türkiye – na kutoa ndege na watu wanaohitajika kuziangusha. Belarus inahifadhi silaha za Russia.

Baadhi ya mataifa hubadilishana ripoti za kijasusi kwa shabaha ya kuamua panapohitaji kulengwa kwa silaha za nyuklia, ama kuruhusu meli zenye silaha za nyuklia kupitia baharini zao na kutia nanga bandarini zao au ndege zenye silaha za nyuklia kuingia anga ya nchi hizo na kuongezwa mafuta katika viwanja vyao vyao ndege.

Matendo yote hayo ya kula njama huendeleza hatari za silaha za nyuklia na kudhoofisha juhudi za kumaliza silaha hizo.

Waandamanaji katika Ujerumani waweka uzio wa kuzunguka kambi ya kijeshi inayohifadhi mabomu ya nyuklia ya Marekani. Picha na: Ralf Schlesener