Silaha za nyuklia zilizopo
Hivi leo, mataifa tisa yana maelfu kadhaa ya silaha za nyuklia, hali ambayo ni tisho la kipekee kwa maisha ya binadamu popote. Mamia ya silaha hizo huwekwa katika tahadhari ya kiwango cha hali ya juu, tayari kutumika ndani ya dakika chache.
Zinahifadhiwa katika vituo vya kurushia makombora, ndani ya ndege za kivita na manowari zinazoweka doria baharini nyakati zote. Baadhi yake zinaweza kusafiri umbali wa maelfu ya kilomita kupitia mabara ili kufikia zinakolengwa.
[FACT]
Ukweli: Mataifa tisa ulimwenguni ambayo yanamiliki silaha za nyuklia yana takribani silaha 12,241.
[/FACT]
Mengi ya mataifa hayo yana mabomu yawezayo kusababisha uharibu mkubwa na maafa mengi kuliko mabomu yaliyoangushwa Hiroshima na Nagasaki katika mwanzo wa enzi ya utumiaji wa silaha za nyuklia. Mabomu kubwa zaidi yana nguvu za zaidi ya tani milioni moja, au megaton moja, ya kemikali ya kisasi inayolipuka, TNT.
Hata mabomu yanayokusudiwa kutumika katika harakati za kivita, yanaweza kusababisha mlipuko wenye nguvu mara 20 zaidi ya bomu lililoangushwa Hiroshima.
Manowari moja yenye silaha za nyuklia inaweza kubeba makombora dazeni moja au zaidi, kila moja ikiwa na kichwa cha nyuklia, yenye uwezo wa pamoja wa kuharibu miji zaidi ya 100.